Mradi mmoja, unaosaidiwa na Kamati ya Kimataifa Uokozi (IRC), inawapatia wakimbizi mikopo midogo midogo kuanzisha biashara.
Mkimbizi raia wa Congo, Enock Gatangi anawahudumiua wateja katika duka la dogo la mboga mboga mjini Nairobi katika ujirani wa Kayole.
Gatangi alikimbia huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo mwaka 2003 na mke wake na mtoto wake na kupatiwa hifadhi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya, ambako aliishi huko kwa miaka 12.
Walihamia mjini Nairobi ambako alifanya kazi kama mlinzi wakazti akiweka akiba ya fedha na kuwa na ndoto ya kuanzisha biashara yake.
Lakini, kama ilivyo kwa wakimbizi wengi, Gatangi alishindwa hata kupata mkopo mdogo kutoka benki.
Baadaye alijiunga na Rangers Family Group, chama cha kuweka na kukopa, ambacho mwezi Januari kilimpatia mkopo wa 4170 ili kumsaidia kufungua duka lake.
Gatangi anasema ana wateja wengi wote wakenya na wacongo. Lakini wateja wake wakuu anasema ni wakenya.
Baada ya mkutano wao wa kila wiki Rangers Family Group huimba nyimbo za kicongo kusherehekea akiba yao.
Wao ni moja ya makundi kama 20 ambayo yanapatiwa msaada na Kamati ya Kimataifa ya Uokozi katika ujirani tofauti mjini Nairobi.
Program ya IRC inaitwa Wakimbizi Afrika Mashariki: Kuboresha Uvumbuzi mmjini kwa Maisha na Maendeleo au Re:Build.
Ni mradi wa miaka 5 kuwawezesha takriban wakimbizi 20,000 walioko mjini wakiwa na biashara zao mjini Nairobi na katika mji mkuu wa Uganda Kampala.
IRC inasema mikopo midogo midogo tayari imewasaidia wakimbizi 260 mjini Nairobi kuweza kuwa wamiliki wa biashara zao.
Boniface Odhiambo ni meneja mradi wa Re:Build anasema ukweli ni kwamba wakimbizi wenyewe wamekabiliwa na changamoto katika misingi ya kupata fursa za kifedha kutoka kwenye taasisi za fedha, mradi umeanzishwa ili kubuni njia za jinsi ya kupata fursa za huduma za kifedha na pia kuboresha juhudi zao za kiuchumi.
Kwa mujibu wa program hii, wakimbizi na wenyeji wanaunda makundi ya wanachama 15 mpaka 30 ambao wanashirikiana kutoa michango.
Fedha zinawekwa sehemu moja kwa kutumia akaunti za kwa njia ya simu ambapo wanachama wanaweza kukopa kama mikopo iudogo midogo kuanzisha na kuendesha biashara ndogo ndogo.
Wanachama mjini Nairobi wanasema mradi umeboresha nafasi yao ya kiuchumi.
Shantalk Zabibu mwenyekiti wa Rangers Family Group huko Kayole anasema kabla ya program kuanzisha walikuwa hawana fursa ya kupata fedha za uwekezaji. Lakini tangu wakati huo waliungana na kuweka rasilimali zao pamoja. Zabibu anasema kama mwanachama anakopa shilingi elfu kumi za Kenya ($90) atapewa. Anasema kama mwanachama mwingine anataka shilingi elfu tano ($45) naye pia atapewa. Zabibu anasema maisha yao yameboreka tangu kujiunga pamoja kama kikundi.
Kenya ni mwenyeji wa kiasi cha wakimbizi na waomba hifadhi 550,000, 87,000 kati ya hao wanaishi mijini.
Ushiriki wao katika uchumi wa Kenya unahusu muingiliano, anasema meneja mradi Odhiambo, na kuongezea “tunapolenga kuwawezesha kiuchumi, tunawapa walio katika mazingira hatarishi au wasio na sauti kupata fursa pia ya kujihisi na kuchangia katika pato la taifa.”
Huku serikali ya Kenya ikipanga kufunga kambi za Kakuma na Dadaab mwezi Julai, macho yote yako kwa mamlaka kuona itachukua hatua gani.
Kuwaingiza wakimbizi katika jamii kama Gatangi kunawafanya kuwa na matumaini kuwa kama kambi zitafungwa, wale wanaisho katika hizo kambi, kama ilivyokuwa kwake, watakuwa tayari na uwezo wa kuishi katika jamii za wakenya.