Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 10, 2025 Local time: 13:57

Siku ya Wakimbizi Duniani: Dunia yakabiliwa na mzozo mkubwa wa ukosefu wa makazi


FILE -Wakimbizi wa Congo wakiwa wanafanya usafi katika Kambi ya Wakimbizi ya Kala wilaya ya Kawambwa's district, Zambia.
FILE -Wakimbizi wa Congo wakiwa wanafanya usafi katika Kambi ya Wakimbizi ya Kala wilaya ya Kawambwa's district, Zambia.

Umoja wa Mataifa unaadhimisha siku ya wakimbizi duniani Juni 20, huku kukiwa na kile ambacho UN inasema mzozo mkubwa sana wa ukosefu wa makazi kuwahi kutokea tangu vita vya pili vya dunia.

Kabla ya Russia kuivamia Ukraine mwezi Februari, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) linasema kulikuwa na tayari watu milioni 80 ambao wamekoseshwa makazi kote duniani. Huku mmiminiko wa raia wa waukraine, ukipandisha idadi hiyo mpaka milioni 100.

Filippo Grandi
Filippo Grandi

Kamishana mkuu wa UNHCRm Filippo Grandi anasema “kukumbuka, hivi sasa wote wanaangazia huko Ukraine kwa kiasi kikubwa, lakini Ukraine inakuja baada ya orodha nyingine ya dharura za awali.”

Ripoti ya shirika hilo kuhusu mwenendo ulimwenguni inasema kwamba mizozo mitano mwaka jana inahusisha takriban asilimia 70 ya watu wasiokuwa na makazi. Wanatokea Syria, Venezuela, Afghanistan, Sudan Kusini na Myanmar.

Wakimbizi wa Rohingya wakiwa katika kambi ya Kutupalong Rohingya huko Cox's Bazar, Bangladesh, June 19, 2022.
Wakimbizi wa Rohingya wakiwa katika kambi ya Kutupalong Rohingya huko Cox's Bazar, Bangladesh, June 19, 2022.

Nchini Afghanistan, watu milioni 24 wanahitaji misaada ya kibinadamu; uchumi uko katika hali mbaya na Taliban imeweka masharti zaidi kwa wanawake na wasichana. UNHCR inasema mashinikizo yote haya yamewasukuma raia wa Afghanistan milioni 2.7 kuondoka nchini.

Peter Kessler ni msemaji wa UNHCR nchini Afghanistan nchini Afghanistan, “kwahiyo, watu wanavuka mipaka, mara nyingine wakiwa na visa lakini wengi wao wakiwa hawana visa na bila ya nyaraka zozote, mara nyingine idadi hiyo inafikia mpaka watu 20,000 kwa siku.”

Watu wengi wanakimbilia nchi jirani. Zaidi ya milioni moja wameondoka nchini Ukraine kwa usalama wao na kuingia nchini Poland.

Msemaji wa UNHCR nchini Poland, Rafal Kostryzynski anasema, watu, wakimbizi, hawakimbilii mbali vya kutosha kutoka kwenye eneo lenye mzozo. Na huwa wanarejea haraka sana na siyo kwa kuchelewa.

FILE - Watoto wa wakimbizi wa Afghanistan wakicheza nje ya eneo la Afghan Basti nje ya mji wa Lahore Juni 19, 2021 katika maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani.
FILE - Watoto wa wakimbizi wa Afghanistan wakicheza nje ya eneo la Afghan Basti nje ya mji wa Lahore Juni 19, 2021 katika maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani.

Kiasi watu milioni 5.6 wamekoseshwa makazi ndani ya nchi na wakimbizi walirejea makwao au kwenye sehemu zao asili walizotoka mwaka 2021.

Lengo la mwaka huu katika siku ya wakimbizi duniani Juni 20 ni haki ya kupata usalama.

Mataifa tajiri yana rekodi mchanganyiko katika kuwakaribisha wakimbizi na waomba hifadhi.

Bwana Grandi anasema watu wanakimbizi kwasababu wana khofu. Siyo tu raia wa Ukraine. “Raia wa Syria wamekimbia mabomu yanayorindima humo, watu huko Tigray nchini Ethiopia nao pia wanakimbia mabomu. Watu katiak eneo la Sahel ama wanakimbia mabomu au mashambulizi holela. Kwahiyo khofu ya ukosefu wa usalama ni sawa, iwe ni raia wa Ukraine au Nicaragu.”

Wahamiaji kutoka Syria REUTERS/Bax Lindhardt/Scanpix A
Wahamiaji kutoka Syria REUTERS/Bax Lindhardt/Scanpix A

Akitikiswa na khofu na ukosefu wa uhakika, Iryna Morykvas alikimbia nchini Ukraine na mtoto wake wa kiume baada ya Russia kuivamia nchi hiyo, alimuacha mume wake nyuma.

“Tulichukua tu vitu muhimu sana na kuvuka mpaka,” anasema Morykvas.

Hivi sasa wako nchini Uholanzi, Morykvas, ni msanii, ameshirikiana na UNHCR katika siku ya wakimbizi duniani kwa kutengeneza emoji ya Twitter.

“Tunapofungua milango yetu kwa watu wenye shida, kwa wakimbizi, kwa mfano, wale ambao wanahitaji msaada, tunafungua mioyo yetu, kwasababu nyumba, ni moyo wa familia.”

Kwa mamilioni ya wakimbiz na wasiokuwa na makazi kote duniani, pia wana matumaini ya kutafuta usalama na kukaribishwa kwa ukarimu.

XS
SM
MD
LG