Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 10, 2025 Local time: 17:57

Watu 7 wauawa katika shambulio dhidi ya kambi ya wakimbizi wa ndani mashariki mwa DRC


Ramani inayoonyesha eneo la Rutshuru, DRC
Ramani inayoonyesha eneo la Rutshuru, DRC

Watu 7 waliuawa katika shambulio kwenye kambi ya waliyohama makazi yao katika eneo la mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lenye ukosefu wa usalama, polisi wamesema Alhamisi

“Usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi, majambazi waliua watu 7, wanaume wanne na wanawake watatu katika kambi ya waliyohama makazi yao ya Rujagati," Patrick Nkundabera, mkuu wa polisi huko Kashuga, wilaya ya Masisi katika mkoa wa Kivu Kaskazini, ameiambia AFP.

“Waasi wa kundi la Nyatura wanaodhibiti eneo hilo wanashukiwa kufanya shambulio hilo," ameongeza.

Kambi hiyo imeshambuliwa kwa mara ya pili tangu ifunguliwe mwaka wa 2008.

Inahifadhi familia 17,000, wengi ni kutoka jamii ya Wahunde na Wahutu.

DRC ina wakimbizi wa ndani milioni 5.3, kituo kinachofuatilia wakimbizi wa ndani na shirika la Norway linalohudumia wakimbizi walisema katika ripoti yao mwezi uliopita.

Kundi la wanamgambo la Nyatura linaundwa zaidi na raia wa Congo wa kabila la Wahutu, ni mmoja ya makundi mengi yenye silaha yanayoendesha harakati katika eneo hilo.

XS
SM
MD
LG