Kenya yaapa kurejesha ubingwa katika mchezo wa Rugby

Mechi ya wanaume kati ya Fiji and Kenya iliyofanyika tarehe 21 January 2023 katika uwanja wa FMG huko Hamilton New Zealand. Picha na MICHAEL BRADLEY / AFP.

Kenya iliapa siku ya Jumanne kurejea katika mfululizo wa World Rugby Sevens, siku chache tu baada ya kushushwa kutoka ngazi ya juu kwa mara ya kwanza katika miongo miwili.

Kenya, ambayo ilianza mfululizo wa dunia kwa mara ya kwanza mwaka wa 1999-2000, na kuwa mshiriki mkuu katika mzunguko wa miaka minne baadaye, ilipata pigo wakati timu ya taifa ya Shujaa iliposhindwa na Canada kwa 12-7 katika mechi ya mchujo ambapo timu hiyo ilishushwa daraja katika mchezo uliofanyika London siku ya Jumapili.

Kushushwa daraja katika mfululizo wa mashindano hayo ya dunia kunamaanisha kuwa Kenya haitafaidika tena na ufadhili kutoka shirikisho la kimataifa la Rugby na kufanya uwezekano wa kuingia katika michuano ya Olimpiki ya mwaka 2024 kuwa magumu.

Lakini bodi mpya ya umoja wa mchezo huo wa Rugby nchini Kenya (KRU) ikiongozwa na Alexander Mutai, ilisema siku ya Jumanne kuwa inataka kurejesha hadhi ya kishujaa katika mfululizo huo wa kimataifa mwaka 2024 na kuhakikisha Kenya inafuzu na kushriki michezo itakayofanyika Paris.

"Katika siku zijazo tutafanya mapitio ya kina ya msimu wa World Series wa mwaka 2022-2023, na kwa kuzingatia matokeo na mapendekezo ya tathmini hii, bodi itafanya maamuzi sahihi na kuelekeza hatua zinazofuata za kuirekebisha timu na kuiweka sawa kuelekea katika mafanikio,"Mutai alisema katika taarifa.
Kenya ilishinda mashindano ya Afrika ya mwaka 2015 na 2019 na kufaulu kushiriki michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016 ya Rio na Tokyo iliyofanyika mwaka 2021.

Chanzo cha taarifa hii ni Shirika la habari la AFP.