Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:09

Kenya: Walioruhusu sukari yenye sumu kuingia katika soko la Kenya kufikishwa mahakamani


Bandari ya Mombasa, kenya PICHA: REUTERS
Bandari ya Mombasa, kenya PICHA: REUTERS

Waliokuwa maafisa wa vitengo katika idara mbambali nchini Kenya, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho Jumatatu, kuhusiana na kashfa ya kuruhusu kwa makusudi uuzaji wa sukari ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa matumizi mengine lakini si salama kwa afya ya binadamu.

Miongoni mwao ni mfanyabiashara mashuhuri aliyehusika na uagizaji wa sukari hiyo, ambaye alikamatwa jumamosi alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, akitokea Dubai.

Kulingana na maafisa wa serikali kontena 40 za sukari yenye sumu, waliuziwa wakenya licha ya kwamba shirika la ubora wa bidhaa lilikuwa limeagiza kwamba sukari hiyo itumike viwandani tu.

Maafisa wa ngazi ya juu wa shirika la ubora wa bidhaa la Kenya na mafisa wa mamlaka ya kukusanya kodi, maafisa wa polisi na maafisaa wa mamlaka ya kilimo na chakula Kenya, ni miongoni mwa watu wanaotarajiwa kufikishwa mahakamani kesho Jumatatu kujibu mashtaka ya maatumizi mabaya ya madaraka na kupanga njama za uhalifu. Karibu watu 20 wamekamatwa.

Mifuko 20,000 ya sukari, kila mfuko ukiwa na uzito wa kilo 50, iliingizwa Kenya mwaka 2018 kutoka Harare, Zimbabwe lakini ikatangazwa kuwa sukari hiyo ina sumu na hivyo si salama kwa matumizi ya binadamu. Sukari hiyo hata hivyo inaripotiwa kwamba ilifunguliwa na kuuziwa wakenya.

XS
SM
MD
LG