Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:51

Kenya yapendekeza kodi kwa bidhaa mbalimbali ili kuziba pengo la kifedha


Rais wa Kenya William Ruto
Rais wa Kenya William Ruto

Kenya inanuia kuanza mpango wa kutoza kodi katika bidhaa mbalimbali ikiwemo kucha bandia, tambi , sarafu za kidijitali na washawishi katika mitandao ya kijamii.

Shirika la habari la AFP linaripoti kwamba hayo ni mapendekezo mapya, ili kuziba pengo la uhaba wa fedha taslimu katika serikali ya Rais William Ruto.

Ruto anataka kurekebisha uchumi wa nchi wenye madeni makubwa aliyorithi kutoka kwa kiongozi aliyemtangulia Uhuru

Kenyatta ambaye alikopa fedha kwa ajili ya kufadhili miradi ya miundombinu iliyokuwa na gharama kubwa.

Licha ya kuahidi kuboresha maisha ya wakenya wengine walio katika hali duni wakati wa kampeni yake mwaka jana , Ruto sasa anachukua hatua za kisiasa ambazo si maarufu za kuongeza kodi.

Serikali ya Ruto imeandaa bajeti ya shilingi trilioni 3.6 ambazo ni sawa na dola za kimarekani bilioni 26.2 kwa mwaka 2023-2024 hukukodi mpya inayopendekezwa ikitarajiwa kuzalisha shilingi bilioni 289.

hata hivyo wakosoaji wameonya kwamba hatua hiyo itaumiza bishara ndogo ndogo ambao ni kiini cha uchumi pamoja na kaya ambazo zinajitahidi kujikimu kimaisha wakati bei za bidhaa zimepanda sana na pia kuna umasikini uliokithiri.

Pauline Akoth anayefanyabiashara ya urembo wa nywele kwa miaka kumi hapa anasema hali ya maisha inazidi kuwa ngumu.

Wakati huohuo Regina Mueni mteja anasema biashara yake ya kusuka nywele inakabiliwa na changamoto kwa sababu ya hali mbaya ya uchumi.

XS
SM
MD
LG