Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:00

Ujenzi wa reli ya SGR kuanza Uganda


Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika hafla ya kutia saini makubaliano ya reli ya SGR, Nairobi Mei 11 2014. PICHA na AFP / Tony KARUMBA.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika hafla ya kutia saini makubaliano ya reli ya SGR, Nairobi Mei 11 2014. PICHA na AFP / Tony KARUMBA.

Uganda ilisema siku ya Alhamisi kuwa ujenzi wa reli ya Standard Gauge (SGR) ambao ulichelewa kuanza utakaogharimu kiasi cha dola bilioni 2.2 utaanza mwaka huu.

Ujenzi wa reli hiyo utakaribisha maendeleo kwa waagizaji na wauzaji bidhaa nje katika nchi isiyo na bandari ambayo kwa muda mrefu walivumilia gharama za juu za usafirishaji.

Mwaka 2015, Uganda iliingia mkataba na kampuni ya Kichina ya Harbour and Engineering Company Ltd (CHEC) kutekeleza mradi huo kwa masharti kwamba kampuni hiyo itasaidia upatikanaji wa ufadhili kutoka serikali ya China kwa ajili ya reli hiyo.

"Serikali ya Uganda... iko katika hatua za mwisho za kuihusisha kampuni ya kituruki ya M/s Yapi Merkezi katika kuiendeleza njia ya reli ya SGR ya mashariki. Mpango ni kuanza ujenzi mwaka huu, "Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ilisema katika taarifa.”

Baada ya miaka mingi ya mazungumzo yaliyokuwa hana tija na Wachina kuhusu ufadhili, hata hivyo mapema mwaka huu Uganda ilisitisha mkataba huo na badala yake walianza mashauriano na kampuni ya Yapi Merkezi ili kutekeleza mradi huo.

Katika taarifa hiyo wizara ilisema "utafutaji wa njia nyingine za ufadhili kutoka Ulaya unaendelea." Haikutaja majina ya wafadhili mahususi kutoka Ulaya ambayo Uganda imekuwa ikiyashawishi.

Njia hiyo ya reli ya Kilomita 273 itatoka mji mkuu wa Uganda, Kampala hadi kwenye mpaka wa nchi hiyo na Kenya , ambako unatarajiwa kuunganishwa na njia ya reli ya Standard Gauge ya Kenya ambayo pia itaiunganisha na bandari ya Mombasa iliyoko katika bahari ya Hindi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG