Shirika hilo lenye makao yake nchini Kenya lilitoa tathmini yake ya sera mbalimbali za kukabiliana na tatizo la taka za plastiki wiki mbili kabla ya mataifa kufanya mkutano mjini Paris wa duru ya pili ya mazungumzo ya kuandaa mkataba wa kimataifa unaolenga kutokomeza taka za plastiki.
Ripoti inaangazia mabadiliko makuu matatu ya soko yanayohitajika ili kuunda uchumi wa endelevu ambao huweka bidhaa zinazozalishwa katika mzunguko kwa muda mrefu iwezekanavyo na kutumika tena, kuchakata na kupanga upya ufungashaji kutoka kwa plastiki hadi nyenzo mbadala.