Wananchi wa Kenya wanasubiri kwa hamu kubwa kusikia ni nani atakae funguliwa mashtaka na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC siku ya Jumatano.
Rais Mwai Kibaki aliitisha kikao cha dharura cha baraza lake la mawaziri siku ya Jumatatu, kujadili namna ya kukabiliana na kesi zitakapofunguliwa.
Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Nairobi, Mwai Gikonyo anaripoti kwamba kulikua na majadiliano makali wakati wa mkutano huo na taarifa iliyotolewa imewahaikikishia wananchi kwamba kutakua na usalama kote nchini.
Mkutano huo wa Mawaziri ulohudhuriwa pia na waziri mkuu Raila Odinga, ulijadili pia juu ya taabia ya balozi wa Marekani nchini Kenya Bw Michael Rineberger. Mawaziri walijadili hasa juu ya wraka za siri zilziochapishwa na Wikileaks ambapo Rineberger alieleza kwamba serikali ya Kenya inaongoza katika ulaji rushwa.
Wakati baraza la mawaziri lilipokua linakutana, polisi wa Nairobi walikua wanawatawanya vijana walokua wqamekusanyika kwenye uwanja wa Kamkunji mjini Nairobi, kwa mkutano uloitishwa na na mbunge wa Ford Kanya Eugean Wamalwa.