Mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu amesema karibu atatoa majina ya watu wanaoshukiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa 2008.
Luis Moreno Ocampo aliuambia mkutano huko Nairobi Alhamisi kwamba atafungua kesi dhidi ya watu sita mashuhuri wanaotuhumiwa kwa kuhusika na ghasia hizo ifikapo Desemba 17.
Amesema ofisi yake itafuatilia kesi mbili kila moja ikihusisha watu watatu na amesema watu majina ya washukiwa hayo yatajulikana.
Kumekuwa na hisia na wasi wasi mkubwa katika siasa za Kenya kwamba yupi anaweza kuwa amelengwa. ICC inaaminika kuwa inachunguza wafanyabiashara maarufu na wanasiasa wakubwa.
Kenya ililipuka ghasia na vita vya kikabila kufuatia uchaguzi uliopiongwa wa mwishoni mwa 2007. Watu wapatao 1300 waliuwawa kabla ya makubaliano ya serikali ya kushirikiana madaraka kati ya rais Mwai Kibaki na mpinzani wake Raila Odinga iliyorudisha amani.