Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 12:02

Wabunge Kenya wajaribu kuzuia kesi za ICC


Wanasiasa wa Kenya wakihudhuria kuapishwa kwa wabunge wa bunge la 10 Kenya 2008.
Wanasiasa wa Kenya wakihudhuria kuapishwa kwa wabunge wa bunge la 10 Kenya 2008.

Mjadala mkali ulijitokeza Alhamisi katika bunge la Kenya kutokana na hoja ya kuiondoa nchi hiyo katika mkataba wa Rome, kwa misingi kwamba haiambatani na katiba.

Wabunge walikua wanajadili ikiwa hoja hiyo iliyowasilishwa na mbunge wa Chepalungu, Issac Ruto, inafuatana na sheria ya nchi. Kufuatana na katiba mpya ya Kenya mikataba yote ya kimataifa inayoidhinishwa inakua ni sehemu ya sheria za Kenya.

Akizungumza na sauti ya amerika PLO Lumumba, mwanasheria na mkuu wa tiume ya kupambana na rushwa Kenya anasema "kila nchi inahakiu ya kujiondoa kutoka Mkataba wa Rome kwa sharti kwamba inatoa ilani ya mwaka mmoja. Hivyo hatua hiyo haitoweza kubadilisha chechote katika mashtaka dhidi ya watu sita walotajwa Jumatano".

Wachambuzi wa kisiasa wanasema mjadala huo ni jaribio la baadhi ya wabunge kuzuia kupelekwa The Hague watu sita mashuhuri wa kenya walotajwa Jumatano na mwendesha mashtaka mkuu wa ICC kuwa wamehusika na ghasia na mauwaji ya baada ya uchaguzi 2008.

XS
SM
MD
LG