Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 05:50

ICC yashitaki waasi wa Sudan

Sudan
Sudan

Waendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC, wanatoa wito kwa waasi wawili wa Sudan kushitakiwa kwa shutuma za kuongoza shambulizi ambalo liliwauwa walinda amani 12 wa Umoja wa Afrika.

Waendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC, wanatoa wito kwa waasi wawili wa Sudan kushitakiwa kwa shutuma za kuongoza shambulizi ambalo liliwauwa walinda amani 12 wa Umoja wa Afrika.

Washukiwa Abdallah Banda Abakaer Nourain na Saleh Mohammed Jerbo Jamus, wanashutumiwa kwa makosa matatu ya uhalifu wa vita kwa shambulizi la mwaka 2007 kwenye kituo cha walinda amani wa Umoja wa Afrika katika mkoa wa Darfur nchini Sudan.

Wanaume hao walijisalimisha wenyewe huko ICC mwezi June na walisema wanataka kusafisha majina yao, japokuwa hakuna aliyekuwepo katika kesi ya Jumatano. Kiasi cha waasi 1,000 walishambulia kituo cha walinda amani cha Umoja wa Afrika kilichopo Haskanita, Darfur mwezi Septemba mwaka 2007, na kuwauwa wanajeshi 12 na kuwajeruhi nane wengine.

XS
SM
MD
LG