Kampuni zapigania haki ya kipekee kuendesha uwanja wa ndege wa Zanzibar

Wafanyakazi wa Dnata wakipakia mizigo katika ndege katika uwanja wa ndege wa Geneva, Uswitz April 1, 2020. REUTERS/Denis Balibouse

Sakata linalohusu utoaji wa haki pekee kwa matumizi ya uwanja mpya wa ndege kwa Wakala wa Taifa wa Safari za Ndege Dubai (Dnata)  uliotolewa na  Mamlaka ya Uwanja wa ndege Zanzibar (ZAA) limechukua taswira mpya Jumanne baada  ya kampuni nyingine kufungua kesi  katika Mahakama  Kuu ya Tanzania.

Kampuni ya Transworld Aviation Limited, imewasilisha kesi katika mahakama kuu ya Tanzania kupinga haki pekee ilizopewa Dnata.

Hata hivyo, mzozo wa kisheria ulijitokeza mara baada ya kesi hiyo kuwasilishwa Jumanne, na kumlazimu jaji Sekela Moshi kujiondoa mapema kusikiliza kesi hiyo.

Kupitia wakili Mdekela kampuni ya Transworld Aviation Peter Mdekela, imesema haina imani na jaji Moshi.

“Tumemuomba jaji anayesimamia kesi hii ajiondoe mwenyewe kwa sababu mlalamikaji hana imani naye, tunamshukuru Mungu jaji amejitoa mwenyewe kutokana na ombi hilo mahsusi,” alieleza.

Mnamo Septemba 14, 2022, ZAA ilitoa muongozo ambao uliwapa wakala hao wa Dubai haki pekee ya matumizi ya uwanja mpya wa ndege ambao umejengwa kwa gharama ya dola za Kimarekani millioni 120.

Amri iliyotolewa na ZAA , imezipa kampuni zilizokuwa zikiendesha shughuli katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar hadi Desemba 1, 2022 kuondoka katika uwanja mpya uliojengwa Terminal III na kuyaagiza mashirika ya ndege kujipanga kufanya kazi na Dnata.

Akizungumza mara baada ya kufungua kesi, Mkurugenzi wa sheria na uwekezaji wa kampuni ya Transworld Aviation Peter Madeleka alisema kuwa Mamlaka ya Anga ya Tanzania (TCAA) na Mwanasheria Mkuu ni watetezi wa kwanza na wapili.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African linalochapishwa Kenya.