Jenerali Andrew Harrison alisema mchakato huo umeanza kupitia mawasiliano yaliyomo kwenye mkataba wa silaha ambao ulisitisha mapigano ya vita vya Korea vya mwaka 1950-53.
Alisema hali ya usalama ya mwanajeshi Travis King ni suala la msingi linaloipa wasiwasi kamandi hiyo, lakini alikataa kutoa maelezo zaidi, akieleza kuwa majadiliano hayo ni nyeti.
Korea Kaskazini imeendelea kukaa kimya kuhusu King, ambaye alivuka mpaka Jumanne iliyopita wakati alikuwa anapaswa kuelekea huko Fort Bliss, Texas.
Maafisa wa Marekani wameeleza wasiwasi wao kuhusu usalama wake na kusema kuwa Korea Kaskazini ilikuwa inapuuza maombi yao kuhusu taarifa za mwanajeshi huyo.
Wachambuzi wanasema Korea Kaskazini ingeweza kusubiri kwa wiki au miezi kadhaa kutoa taarifa ya maana kuhusu King ikijaribu kurefusha matakwa yao na kuongeza shinikizo kwa juhudi za Marekani katika kufikia kuachiwa kwake.
Baadhi wanasema Korea Kaskazini inaweza kujaribu kuvutana kupata maridhiano ya Washington, kama vile kuweka masharti ya kuachilike, kwake, kwa Marekani kupunguza shughuli zake za kijeshi na Korea Kusini.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP