Makamu Rais wa Taiwan, William Tai, mgombea wa kwanza katika uchaguzi wa urais wa kisiwa hicho uliopangwa kufanyika Januari, alitangaza wiki hii kwamba ana panga kufanya ziara nchini Marekani mwezi ujao akiwa njiani kuelekea Paraguay na kusababisha maandamano ya haraka kutoka China.
Beijing inapinga hatua yeyote itakayoweza kuongeza hadhi ya kimataifa kwa Taiwan na imeahidi kuzuia safari hiyo isifanyike.
Wachambuzi wanasema wakati suala hilo halionekani kufanikiwa kwa China mpango wa safari hii unaonekana kuwa jaribio ambalo tayari limeleta uhusiano wenye mvutano kati ya Beijing na Marekani.
Forum