Waokoaji walikuwa wakitafuta waathiriwa kwenye vifusi vya jengo la ghorofa tano katika mji wa George huko Afrika Kusini lililoporomoka siku ya Jumanne
Waokoaji wamesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuwa wamewasiliana na watu 11 waliokwama kwenye vifusi vya jengo hilo lililokuwa likijengwa na kuua watu watano na 50 bado hawajapatikana.
Colin Deiner, mkuu wa usimamizi wa maafa katika Jimbo la Western Cape, alisema walikuwa wakilenga maeneo ambayo wamekuwa wakisikia sauti za watu.
Maafisa wa mji huo wamesema wafanyakazi 75 wa ujenzi walikuwa kwenye eneo la jengo hilo lilipoporomoka kwa sababu zisizojulikana siku ya Jumatatu.
Rais Cyril Ramaphosa ametoa salamu za rambirambi kwa familia za waliofariki kwenye mkasa huo na kuamuru uchunguzi ufanyike.