Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, wengi wa waliokwama kwenye vifusi vya jengo hilo ni wajenzi. Kufikia Jumatatu jioni mwili mmoja ulipatikana wakati manusura watatu waliokolewa, huku timu za uokozi zikiendelea na shughuli za uokozi.
Matukio ya majengo kuanguka ni suala la kawaida nchini Nigeria ambako sheria za ujenzi hazijingatiwi inavyohitajika. Mamlaka za mji wa Lagos zimesema kwamba jengo hilo lilikuwa na gorofa 22, na kwamba wanaendelea na ukaguzi wa majengo yalioko karibu ili kutadhmini iwapo yaliathiriwa. Jengo hilo linasemekana kuwa sehemu ya majengo mengine matatu yaliokuwa yakijengwa na kampuni ya Fourscore Homes.