Mwakilishi mwengine ambaye ni mpya amejiunga katika Baraza la Wawakilishi, ambaye aligombea uongozi wa ofisi ya umma kwa mara ya kwanza 2018.
Lakini kuhusu ushawishi wa mitandao ya kijamii, Mwakilishi Mdemokrat wa New York Alexandria Ocasio-Cortez ni dhahiri kuwa anaongoza na kumpita hata Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi kwa wafuasi wanaofuatilia akaunti yake ya Twitter, hii ni katika wiki iliyopita.
Baraza hilo la kikao cha 116 ni lenye watu mchanganyiko zaidi katika historia ya Marekani na walio katika umri mdogo. Wawakilishi 25 wa Baraza la Wawakilishi jipya ni (millennials ) vijana, ikiwa ni sehemu ya kizazi kilicho zaliwa 1980 na pia wanawepesi wa kutumia mitandao ya kijamii zaidi.
Ocasio-Cortez anaongoza kikundi hiki cha wawikilishi wapya, habari zao zikigonga vichwa vya habari kutokana na ukosoaji wao wenye mivutano ya kisiasa, akionyesha picha akiwa hewani kupitia simu yake, ikionyesha anavyo pika nyumbani kwake, na kuzungumza juu ya mipango yake ya “Green New Deal.”
"Green New Deal" ni pendekezo la programu ya kuchochea ukuwaji wa uchumi nchini Marekani inayolenga kuleta usawa kiuchumi na kutafuta ufumbuzi wa mabadiliko ya tabia nchi.
Picha hizo za video anazoposti mwakilishi huyo zinawapa wapiga kura nafasi ya kujua sehemu ya maisha yake binafsi, wakati huo akitoa muhtasari wa yale ambayo yamejificha kuhusu maisha kama mwakilishi anaye jiunga kwa mara ya kwanza na Baraza la Wawakilishi.
Lakini Wademokrat siyo kwamba wao pekee kama Wawakilishi kuwa wazoefu wa mitandao ya jamii. Utumiaji wa akaunti ya twitter unaofanywa na Rais Trump umeleta mapinduzi katika safu hii na kufanya iwe ni nafasi ya kujadili masuala ya sera yanayotokea, akiwashawishi wawakilishi wa Warepublikan juu ya uwezo wa mitandao hiyo kuweza kufikisha ujumbe wao kwa njia mpya..