Jeshi la Somalia limemuua kamanda mmoja wa kundi la Al Shabaab katika operesheni ya kijeshi, radio ya serikali ya Somalia ilitangaza siku ya Alhamisi.
Kamanda aliyeuawa ambaye ni maarufu kwa jina la Ahsraf Azmi Abu Hamdan, ni raia wa Nepal, ambaye alikuwa mkufunzi mwandamizi katika kundi hilo lenye msimamo mkali; wanayodai kuwa ni ya Kiislam.
Kulingana na taarifa ya radio ya serikali ya Somalia, kamanda huyo aliuawa katika operesheni ya kijeshi iliyofanyika katika jimbo la Juba kusini mwa Somalia.
Pia taarifa zinaeleza kuwa wapiganaji wa 3 wa al-Shabaab waliuawa katika operesheni hiyo.
Al Shabaab imekuwa ikifanya harakati za kuindoa serikali kuu ya Somalia tangu mwaka wa 2008, ili kuweka uongozi wake wenye sheria kali za Kiislamu.