Jeshi la Myanmar lashambulia kabila la waliowachache kudhibiti eneo

Wapiganaji wa kikundi cha ukombozi cha People's Liberation Army PLA wakiwa wamembeba moja wa wapiganaji aliyejeruhiwa katika mapambano yao dhidi ya Utawala wa Kijeshi wa Myanmar karibu na Mkoa wa Sagaing, Myanmar Novemba 23, 2023. REUTERS/Stringer

Jeshi la Myanmar linaendelea na mashambulizi yanayohusisha ndege za kivita ili kurejesha udhibiti wa mji muhimu kutoka kwa kundi la watu wachache wenye silaha, wapiganaji wake na wakaazi wanasema.

Watu waliokoseshwa makazi kutokana na ghasia za hivi karibuni katika mji wa Pauktaw wakisikiliza habari kupitia radio kwenye kambi ya wakimbizi Waislam ya Owntaw Novemba 1, 2012. Wachunguzi wa haki za binadamu wa UN wameitaka Myanmar Jumatano kusitisha ghasia za mauaji.

Jeshi la Arakan lilihamia Pauktaw, mji wa watu 20,000 karibu na bandari muhimu ya kina kirefu katika mji mkuu wa jimbo la Rakhine magharibi, mnamo Novemba 15.

Ilifungua mkondo mpya katika mashambulio kwa makabila madogo kaskazini mwa Myanmar ambayo yameghadhibisha jeshi la serikali, kukata njia za biashara kuelekea China jirani na kusababisha zaidi ya watu 330,000 kuhama makazi tangu mwezi uliopita.

Pauktaw imekuwa moja ya maeneo yanayo zozaniwa na wakaazi waliowasiliana na AFP siku ya Jumatano waliripoti mapigano makali ndani na nje ya mji huo, ambao ni kilomita 25 kutoka Sittwe, mji mkuu wa jimbo hilo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.