Jenerali al-Burhan wa Sudan aitembelea Eritrea

Rais wa Eritrea Isaias Afwerki alipomkaribishwa na Jenerali Abdel Fattah Al-Abdelrahman Burhan alipowasili Khartoum, Sudan Septemba 14, 2019. Picha na REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan wa Sudan, aliye vitani katika muda wa miezi mitano iliyopita na wanamgambo wa kikosi cha dharura cha Rapid Support Forces, anaitembelea nchi jirani ya Eritrea siku ya Jumatatu, maafisa wa nchi zote mbili wametangaza.

Hii ni safari ya nne nje ya nchi kwa Burhan katika kipindi cha muda wa wiki mbili, kiongozi huyo ambaye aliyanyakua madaraka katika nchi hiyo ya kaskazini mashariki kwa Afrika wakati wa mapinduzi ya mwaka 2021.

Tangu Agosti 29, Burhan amezitembelea nchi za Misri, Sudan Kusini na wiki iliyopita Qatar. Wataalamu wanasema hii ni sehemu ya juhudi za kubainisha sifa zake za kidiplomasia endapo kutakuwa na mazungumzo ya amani ya kumaliza vita nchini mwake.

Waziri wa Habari wa Eritrea Yemane Meskel alitangaza kwenye mtandao wa X, uliokuwa ukijulikana kama Twitter, kwamba Burhan amewasili Asmara siku ya Jumatatu "kwa ziara ya kikazi," na kuchapisha picha yake akiwa ameketi pembeni mwa rais wa nchi hiyo Isaias Afwerki.

Viongozi hao watajadili "hatma ya baadaye ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kuuimarisha," ilisema taarifa kutoka ofisi ya Burhan kwa vyombo vya habari hapo awali.

Eritrea, ambayo inapakana na Sudan katika eneo la kusini-mashariki, ni moja ya nchi jirani adimu ambazo hazijapokea mkimbizi yeyote kati ya zaidi ya milioni moja wanaokimbia vita, kwa kuwa mpaka huo umefungwa tangu mwaka 2019.

Eritrea ni moja ya nchi iliyotengwa zaidi duniani.

Afwerki alishiriki katika mkutano uliofanyika mjini Cairo katikati ya Julai na wakuu wa mataifa jirani na Sudan, wakilaani " vita ilivyoanzishwa bila sababu" nchini Sudan.

Mapigano yaliyoanza nchini humo Aprili 15 kati ya jeshi na Kikosi cha Msaada wa Dharura (RSF) cha Jenerali Mohamed Hamdan Daglo, vita ambavyo vimesababisha vivo vya watu takribani wa 7,500, kulingana na makadirio ya kihafidhina kutoka shirika lisilo la kiserikali la the Armed Conflict Location & Event Data Project.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.