Watu waliokimbia wanajumuishwa kwenye idadi ya karibu watu milioni 2.8 ambao tayari walihama makazi yao kutoka mji mkuu wa Sudan ambao ulikuwa na takriban wakazi milioni 5 kabla ya vita kuzuka Aprili 15 kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha dharura cha Rapid Support Forces ( RSF).
Mkazi ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu za kiusalama ameiambia AFP kwamba “mamia ya familia zilikimbia kutoka Ombada”, wilaya ya mji pacha wa Khartoum wa Omdurman.
Jeshi la Sudan linadhibiti anga juu ya mji wa Khartoum na limefanya mara kwa mara mashambulizi ya anga, huku wapiganaji wa RSF wakidhibiti mitaa ya Khartoum.
Kundi la wanaharakati wa Ombada Jumanne jioni lilisema jeshi lilishambulia kwa makombora na ndege zisizo na rubani” ngome za wanamgambo wa RSF.
“Mashambulizi ya jeshi hayakupiga malengo waliyotarajia na hivyo raia 19 waliuawa,” kundi hilo limeongeza katika taarifa yake kwenye Facebook.
Forum