Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 21:16

Bwawa la Ethiopia lakamilika kujazwa maji


Bwawa kubwa la Grand Renaissance nchini Ethiopia
Bwawa kubwa la Grand Renaissance nchini Ethiopia

Ethiopia ilisema Jumapili kwamba imekamilisha awamu ya nne, na ya mwisho, ya kujaza maji kwenye bwawa kubwa la kuzalisha umeme, kwenye mto wa Blue Nile, mradi ambao Misri na Sudan zimepinga kwa muda mrefu.

Ujenzi wa bwawa la Grand Ethiopian Renaissance, (GERD), lenye thamani ya dola bilioni 4 ulianza 2011 na Ethiopia inauona mradi huo kuwa muhimu katika kuimarisha maendeleo yake ya kiuchumi. Misri na Sudan, hata hivyo, zinauchukulia mradi huo kuwa tishio kubwa kwa vyanzo vyao muhimu vya maji.

"Hongera kwa wote kwa kujazwa kwa Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance. Ustahimilivu wetu kama taifa dhidi ya hatari zote umeleta tija," afisi ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed iliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, ambao awali ulijulikana kama Twitter, hapo ya Jumapili.

Ukikadiriwa kuwa na nguvu za zaidi ya megawati 6,000, Ethiopia inaona mradi wa GERD kama jukwa la azma yake ya kuwa muuzaji mkubwa zaidi wa umeme barani Afrika.

Forum

XS
SM
MD
LG