Watafiti wanalenga kuchanja zaidi ya watu 800 waliojitolea kwa chanjo moja ya Pfizer-BioNTech, ikifuatiwa na wiki nne au 12 baadaye ya chanjo ya nyongeza iliyo tengenezwa kwa pamoja na kampuni ya AstraZeneca na Chuo Kikuu cha Oxford, au kinyume chake.
Chanjo hizo zilitengenezwa na teknolojia tofauti - chanjo ya Pfizer kupitia messenger RNA (mRNA), wakati chanjo ya AstraZeneca-Oxford ni ya virusi vya adenovirus, au virusi vya homa ya kawaida.
Maafisa wa afya wanasema ikiwa chanjo mbili zilizo tengenezwa na teknolojia tofauti zina uwezo wa kutumiwa kwa kubadilishana, inaweza kuruhusu mabadiliko zaidi katika kampeni za chanjo ulimwenguni.