Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:20

Uingereza inapanga kufanya majaribio zaidi ya aina mpya ya virusi


Waziri wa afya wa Uingereza, Matt Hancock, Januari 13, 2021.
Waziri wa afya wa Uingereza, Matt Hancock, Januari 13, 2021.

Matt Hancock anasema maafisa wa afya wa Uingereza kwa kushirikiana na serikali za mitaa wanaenda nyumba hadi nyumba kuwapima watu katika maeneo yao

Waziri wa afya wa Uingereza, Matt Hancock, amesema Jumatatu kesi 105 za aina mpya ya virusi vya Corona vilivyogundulika kwa mara ya kwanza nchini Afrika kusini vimegundulika nchini humo na kesi 11 kati ya hizo hazina uhusiano wowote na safari za kimataifa.

Akizungumza kutoka jengo la ofisi za serikali nchini humo, Hancock amesema maafisa wa afya wanapanga kuwafanyia majaribio watu 80,000 kutoka maeneo ya nchi nzima pamoja na kuwatenganisha ili kuzuia kusambaa kwa aina hiyo mpya ya virusi.

Kiongozi huyo amesema kuongezeka kwa upimaji mpya kunalenga kwenye maeneo hayo mahala ambako aina mpya ya virusi iligunduliwa na kwamba matokeo ya kila kesi yanafuatiliwa kwa makini. Anasema maafisa wa afya, kwa kushirikiana na serikali za mitaa wanaenda nyumba hadi nyumba, kuwapima watu katika maeneo hayo.

XS
SM
MD
LG