Kulingana na vyanzo vya habari uamuzi huo ulikuwa na mapungufu kwa matarajio ya wanaharakati, lakini bado unaonekana kama hatua ya kusonga mbele.
Hukumu ya mahakama ya wilaya ya Fukuoka ilitolewa wiki moja baada ya mahakama nyingine ya wilaya kusema ni kinyume cha katiba kupiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja.
Hukumu hiyo iliongeza matumaini ya mabadiliko miongoni mwa jumuiya ya LGBTQ nchini Japan, ambalo ni taifa pekee la nchi saba kuu duniani ambalo halina sheria ya kuwalinda watu wa ndoa za jinsia moja.
Maamuzi matano kuhusu ndoa za watu wa jinsia moja yametolewa nchini Japan katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, mawili yakihitimisha kwamba marufuku hayo yalikuwa kinyume na katiba, moja ikisema sivyo, na mawili, ikiwa ni pamoja na la Alhamisi, yakiunga mkono marufuku hiyo lakini kuibua masuala mengine ya haki
Mahakama ya Tokyo mwaka jana iliidhinisha marufuku hayo lakini ilisema ukosefu wa ulinzi wa kisheria kwa familia za jinsia moja ulikiuka haki zao.