Israeli na Ugiriki kubuni programu ya AI kupambana na moto wa misituni

Ndege ya Helikopta ikijaribu kuzima moto wa msituni

Ugiriki inashirikiana na Israeli katika kubuni teknolojia ya program ya kompyuta maarufu kama AI, ambayo itasaidia kutambua mapema moto hatari wa nyika, waziri mkuu wa Ugiriki alisema Jumatatu.

Baada ya mazungumzo na mwenzake wa Israeli Benjamin Netanyahu na Rais wa Cyprus, Nikos Christodoulides, katika mji mkuu wa Cyprus wa Nicosia, Kyriakos Mitsotakis pia alisema kuwa Israeli inaweza kukubaliwa katika Umoja wa Ulaya linapokuja suala la mipango ya ulinzi wa raia, ili kuratibu vyema juhudi za kuzima moto.

Israeli na Cyprus ni miongoni mwa nchi kadhaa ambazo zimetuma ndege na wafanyakazi wa kuzima moto kusaidia kupambana na moto wa nyika nchini Ugiriki, ambao uliteketeza sehemu kubwa ya misitu katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, ukiwemo moto mkubwa zaidi katika ukanda wa Umoja wa Ulaya ambao ulisababisha vifo vya watu 20.

Mitsotakis alisema Ugiriki inaweza kutumika kama msingi wa kuthibitisha teknolojia ya AI ya Israeli katika kutambua mapema moto wa nyika.