Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 02:21

Watu 73 wafariki baada ya moto kuteketeza jengo la makazi nchini Afrika Kusini


Jengo lililotekezwa na mto katikati ya mji wa Johannesburg, Agosti 31. Picha ya AP
Jengo lililotekezwa na mto katikati ya mji wa Johannesburg, Agosti 31. Picha ya AP

Moto ulioteketeza jengo la ghorofa tano ambalo liligeuzwa kuwa makazi haramu uliwaua zaidi ya watu 70 wakiwemo watoto katikati ya mji wa Johannesburg leo Alhamisi, idara ya huduma za dharura katika mji huo wa Afrika Kusini imesema.

Watu wengine 52 walijeruhiwa katika kile ambacho kinaonekana kuwa ajali mbaya zaidi ya moto duniani katika miaka ya hivi karibuni.

Miili ilipatikana ikiwa imerundikana kwenye mlango wa usalama ambao ulikuwa umefungwa na hivyo kuwazuia watu kutoroka moto huo, afisa mmoja amesema.

Maafisa wa mji huo wamesema jengo hilo lililopo katika eneo ambako hakuna uhalifu liligeuzwa kuwa makazi haramu baada ya kutelekezwa.

Mkazi mmoja amesema,wengi waliokuwa wanaishi ndani ya jengo hilo ni raia wa kigeni.

Msemaji wa idara ya usimamizi wa huduma za dharura Robert Mulaudzi amesema “Sasa tuna vifo 73 na majeruhi 52 ambao walipelekwa kwenye vituo mbalimbali vya huduma za afya kwa ajili ya matibabu zaidi.”

Forum

XS
SM
MD
LG