Wakati sistisho la mapigano linatekelezwa kulikuwa na msururu wa magari yaliyokuwa yanaelekea kusini mwa Lebanon ambako kwa miezi kadhaa kulikuwa na mapigano makali na kuwalazimisha watu kuhama nyumba zao.
Jeshi la Israel liliwaonya watu kukaa mbali na vijiji vyao ambako iliwahi kuamuru kuondoka.
Wakati huo huo wanajeshi wa ziara wa Lebanon wamepelekwa kusini mwa nchi baada ya kufikiwa sitisho la mapigano kuanza.
Magari ya jeshi la Lebanon yameingia katika Barabara za Tyre na Burj al-Shemali kusini mwa Lebanon, yakipishana na magari ya kiraia yakiwa wamebeba mizigo huku watu wakirejea kwenye nyumba zao baada ya vita kusitishwa wakati jeshi likiongeza idadi ya wanajeshi.
Marekani pamoja na Ufaransa wamekuwa na jukumu kuu katika kusimamia kufikiwa kwa suluhu ambapo baraza la mawaziri la usalama la Israel liliidhinisha jumanne jioni
Rais wa Marekani Joe Biden aliita sitisho la mapigano ni hatua muhimu kumaliza ghasia huko mashariki ya kati. Alisema Iran na washirika wake, hezbolah huko Lebanon na wanamgambo wa Hamas huko Gaza wamelipa gharama kubwa kwa sana kwa zaidi ya mwaka mmoja wa mapiano na wanajeshi wa Israel.
Baadhi ya taarifa ya habari hii inatoka Shirika la habari la Reuters