Iran imepokea kurejeshwa kwa vikwazo dhidi yake na Marekani kwa kufanya mazoezi ya jeshi la anga.
Rais wa Iran Hassan Rouhani amekiri kwamba taifa lake linakabiliwa na kile alichokiita ‘hali ya vita vya kiuchumi” hatua ambayo inaongeza mvutano baina ya Marekani na Iran.
Vikwazo hivyo vinamaliza mafao yote ya kichumi ambayo Iran ilipata baada ya makubaliano ya mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 na mataifa makubwa duniani.
Wachambuzi wa kisiasa wanasema kuwa vikwazo vipya vya Marekani vitaumiza zaidi sekta ya mafuta ya Iran, ambayo ni muhimu kwa nchi hiyo katika kuinua uchumi wake.
Sarafu ya Iran imepungua thamani kwa kiwango kikubwa na kusababisha bei za bidhaa muhimu nchini humo kupanda kwa kasi.