Maelfu ya watu waliingia kwenye mitaa ya Tehran, mji mkuu wa nchi hiyo mapema Ijumaa bila ya kufuata kanuni za afya zinazowataka watu kutokaribiana ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya ugonjwa huo.
Watu takribani wawili wanaripotiwa kufariki katika tetemeko hilo leo katika mji mkuu wa Tehran.
Wakati huo huo Australia ilitangaza mpango wa hatua tatu leo Ijumaa wa kuanza taratibu za kufungua tena shughuli za umma baada ya kufunga shughuli zote ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.
Wakati majimbo mbalimbali nchini Marekani yanaendelea kupambana kupata vifaa vya kupima COVID-19 kwa ajili ya wakaazi wake, White House inatangaza Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu wa Rais Mike Pence watakuwa wakifanyiwa vipimo vya COVID-19 kila siku.
Hatua hiyo inafuatia maambukizi ya mfanyakazi mmoja kwenye makazi ya Rais.
Kabla ya mfanyakazi huyo kuwa mgonjwa, viongozi hao wawili wa Marekani walikuwa wakipimwa mara moja kwa wiki.