Iran yadai kulinda maslahi yake wakati wa utawala wa Trump

Msemaji wa serikali ya Iran Fatemeh Mohajerani akitoa maoni kuhusu sera za Iran. Picha na Reuters

Iran imesema itafuata chochote kinacholinda maslahi yake, msemaji wa serikali Fatemeh Mohajerani alisema Jumanne , alipoulizwa kama kuna uwezekano wa kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na utawala wa Trump.

Hata hivyo hakuna ripoti zozote kwamba Donald Trump au timu yake wanapanga aina yoyote ya mazungumzo wakati akijiandaa kurejea tena katika muhula mwingine kama rais wa Marekani.

Trump aliiondoa Marekani katika mkataba wa nyuklia wa Iran wa mwaka 2015 na mataifa yenye nguvu duniani katika muhula wake wa uongozi mwaka 2018 na kuiwekea tena vikwazo ambavyo viliathiri vibaya Uchumi wa Iran.

Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Washington na Tehran kuhusu kufufua mpango wa nyuklia yalianzishwa chini ya utawala wa Rais Joe Biden lakini yalikwama.

Iran bado ni sehemu rasmi ya makubaliano hayo lakini imepunguza nia yake ya dhati kuheshimu kutokana na vikwazo vya Marekani vilivyowekwa tena na jamhuri ya kiislamu.