Sharmahd mwenye uraia pacha wa Iran na Ujerumani, na pia kiongozi wa upinzani alituhumiwa kupanga shambulizi la bomu la 2008, kwenye msikiti mmoja mjini Shiraz. Familia yake inakanusha madai hayo ikidai kuwa Iran ilimteka nyara 2020 wakati akiwa Dubai.
Sharmahd mwenye umri wa miaka 68 amekuwa akiishi Marekani ambapo alikuwa msemaji wa kundi la Tondar, ambalo hulenga kurejeshwa kuwa utawala unaoungwa mkono na Magharibi nchini Iran, na uliokuwepo kabla ya mageuzi ya Kiislamu 1979.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock, amekemea mauaji hayo kwa maneno makali, akisema kuwa Sharmahd alipelekwa Iran baada ya kutekwa Dubai na kisha kushikiliwa kwa miaka kadhaa bila kushitakiwa, na kisha kuuwawa.
Amesisitiza kuwa serikali ya Ujerumani iliweka bayana kwa Tehran mara kadhaa kwamba kuuwa raia ya Ujerumani kungekuwa na madhara yake.
Forum