Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 12:36

Mkuu wa shirika la UN linalofuatilia silaha za nyuklia anaitembelea Iran


Rafael Grossi, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalofuatilia silaha za nyuklia (IAEA).
Rafael Grossi, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalofuatilia silaha za nyuklia (IAEA).

Grossi ataenda Iran kujadili program yake ya nyuklia na anatarajia kufanya kazi vyema na rais mteule wa Marekani Donald Trump.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kufuatilia silaha za nyuklia Rafael Grossi ataitembelea Iran Jumatano ijayo na kuanza mashauriano na maafisa wa Iran siku inayofuata, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti Jumapili.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki-IAEA alisema siku ya Jumatano kwamba huenda akaelekea Iran katika siku zijazo kujadili program yake ya nyuklia inayozozaniwa, na kwamba anatarajia kufanya kazi kwa ushirikiano na rais mteule wa Marekani Donald Trump.

Masuala ya muda mrefu kati ya Iran, IAEA na mataifa ya magharibi yanajumuisha Tehran kuwazuia wataalam wanaohusika na usindikaji wa uraniam kutoka kwa timu za ukaguzi za IAEA nchini humo, na kushindwa kwake kwa miaka kadhaa kuelezea uwepo wa uraniam iliyogundulika katika maeneo ambayo hayajatangazwa.

Iran pia imeongeza harakati za nyuklia tangu mwaka 2019, baada ya rais wa wakati huo Trump kuachana na makubaliano ya mwaka 2015 ambayo Iran iliyafikia na mataifa yenye nguvu duniani ambayo yalizuia urutubishaji wa nyuklia ulioonekana na magharibi kama juhudi za kubadilisha ukuaji wa uwezo wa silaha za nyuklia, na kurejesha vikwazo vikali vya Marekani dhidi ya Jamhuri hiyo ya Kiislamu.

Forum

XS
SM
MD
LG