Muungano unaoongozwa na Marekani nchini Iraq umeeleza Jumatano kumefanyika shambulizi la roketi lililolenga kambi ya jeshi ambayo inatumiwa na vikosi vya muungano.
Msemaji wa muungano huo Kanali Wayne Marotto amesema kulikuwa na roketi 10 zilizo fyatuliwa katika kambi ya jeshi la anga la Al-Asad.
Hakuna taarifa zozote za vifo mpaka hivi sasa. Shambulizi hilo limefanyika baada ya kupita wiki mbili toka kutokea tukio lingine la roketi kurushwa katika kambi ya jeshi iliyopo kaskazini mwa Ifaq na kumuua mkandarasi ambaye ni raia ina kujeruhi wanajeshi wa Marekani.
Mashambulizi ya Febuari 16 yalichochea Marekani kufanya mashambulizi ya anga yakilienga Syria ambapo Pentagon ilieleza kuwa ndiko kuliko pangwa mashambulizi mfululizo katika kambi za jeshi nchini Iraq.