Baada ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kukamilisha mageuzi miaka kadhaa ya kifedha chini ya mpango wa kuzipunguzia madeni nchi maskini maarufu kama Heavily Indebted Poor Countries Initiatives au HIPC.
Mpango huo ulianzishwa na IMF na Benki ya Dunia mwaka 1996 ili kuzisaidia nchi maskini kuhimili madeni.
Katika taarifa ya IMF na Benki ya Dunia zimesema upunguzaji wa madeni “utasaidia katika upatikanaji wa rasilimali za ziada za kifedha na kwamba utaisaidia Somalia kuuimarisha uchumi wake na kupunguza umaskini na kuboresha uzalishaji wa ajira”
“Baada ya HIPC kukamilisha hatua, deni la nje la Somalia limeshuka kutoka asilimia 64 ya pato la taifa la mwaka 2018 mpaka chini ya asilimia sita ya pato la taifa ifikapo mwisho wa mwaka huu wa 2023” taarifa hiyo aliongeza.
Serikali ya Somalia imefurahishwa nai msamaha huo wa madeni.
“Ni hatua kubwa, na tunajivunia hasa” waziri wa fedha Bihi Egeh aliiambia Sauti ya Amerika katika mahojiano.
Somalia ni nchi ya 37 kukamilisha mchakato wa HIPC ambao umekuwa ukitumika tangu mwaka 1996.
Madeni hayo yanaanzia mwaka 1991, wakati rais wa zamani Mohamed Siad Barre alipoondolewa madarakani, na uchumi wa nchi kuporomoka.
Meneja wa Kanda wa Benki ya Dunia Kristina Svensson amesema hatua hiyo inaipa Somalia mwanzo mpya katika safari yake ya uchumi.
Baraza la mawaziri la Somalia liliidhinisha zaidi ya dola bilioni moja kwa bajeti ya mwaka ujao, kiwango kikubwa cha bajeti yake ni misaada kutoka nje, wakati serikali ya Somalia bado haijakusanya mapato ya nchi nzima. Kwa sasa kiwango kikubwa cha mapato ya serikali kinatoka katika bandari ya Mogadishu na uwanja wa ndege.