Hayo ameyasema wakati alipokuwa akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Kenya. Taifa hilo la Afrika Mashariki lenye uchumi mkubwa limekuwa likikabiliwa na changamoto kadhaa, zikiwemo uhaba wa fedha katika serikali, mfumuko wa bei za bidha, pamoja na kushuka kwa thamani ya sarafu, hali ambayo imeongeza gharama za ulipaji madeni.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, kufikia Juni Kenya itakuwa na deni la zaidi ya dola bilioni 66, kulingana na takwimu za wizara ya fedha, sawa na takriban thuluthi mbili ya mapato ya ndani.
Ruto hata hivyo hakutoa takwimu zozote kuhusu viwango vya sasa vya deni, lakini amesema pato la jumla la ndani limekua kwa asilimia 5.4 katika miezi sita iliyopita.
Forum