Sudan ilifunga huduma ya internet Oktoba 25 kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.
Pia iliuondoa madarakani utawala wa kiraia uliyokuwa unaongoza taifa hilo katika kipindi cha mpito tangu kupinduliwa kwa Omar al-Bashir.
Mahakama moja Jumanne iliamuru kampuni za Zain, MTN na Sudani, kurudisha huduma za internet lakini shirika linalofuatilia uhuru wa matumizi ya internet la Netblocks, limesema kwamba bado hakuna huduma ya internet nchini humo.
Wanaharakati wa kudai mabadiliko, waliofanikiwa kuandaa maandamano ya awali, wamefanikiwa kuandaa maandamano ya kutaka kurejeshwa utawala wa kiraia bila ya kuwepo huduma ya internet. Wameitisha maandamano mengine Jumamosi, Novemba 13.