Chama cha Ramaphosa cha African National Congress (ANC), ambacho kimetawala tangu Rais Nelson Mandela kukiongoza kwelekea ushindi katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia baada ya ubaguzi wa rangi mwaka 1994, kinaelekea katika kampeni yake, yenye ushindani mkubwa zaidi.
Ukusanyaji wa maoni tofauti tofauti unaonyesha kuwa huenda kikapoteza wingi wake wa wabunge katika kura inayotarajiwa kupigwa kati ya Mei na Agosti mwaka huu, na kulazimika kuunda muungano wa vyama ili kwendelea kushikilia mamlaka.
Afrika Kusini inakabiliwa na uhaba mkubwa wa umeme na mzozo wa vifaa katika kampuni yake ya operesheni za reli na bandari ya Transnet, ambayo imekandamiza shughuli za biashara na kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi, katika nchi hiyo iliyoendelea zaidi kiviwanda barani Afrika.
Katika hotuba yake ya kila mwaka ya Hali ya Taifa, Ramaphosa alikubali matatizo haya. Lakini alitoa masuluhisho machache mapya, na mara kwa mara alidhihakiwa na wabunge.
"Hotuba yake haikueleza jinsi atakavyoshughulikia changamoto nyingi zinazokabili nje," mmoja wa waliohudhuria alwaambia waandishi wa habari muda mfupi baada ya hotuba hiyo.