Hemeti afanya mazungumzo na viongozi wa Ethiopia

FILE PHOTO: Bwawa kubwa la Ethiopia lilioko katika Mto Blue Nile, Renaissance Dam.

Kiongozi wa juu wa pili mwenye nguvu nchini Sudan amekutana na waziri wa ulinzi wa Ethiopia Jumamosi katika ziara ya nadra mjini Addis Ababa kufanywa na afisa kutoka Khartoum. Ziara imefanyika wakati kukiwa na mivutano ya mpakani, maafisa wamesema.

Mohamed Hamdan Daglo, anayejulikana sana kama Hemeti, ambaye ni wapili madarakani katika baraza la uongozi la Sudan, atakuwepo nchini Ethiopia kwa siku mbili na atakutana β€œna maafisa kadhaa wa Ethiopia,” shirika la habari la serikali ya Sudan, SUNA, limeripoti.

Kiongozi huyo alilakiwa uwanja wa ndege wa Addis Ababa na Waziri wa Ulinzi wa Ethiopia Abraham Belay, taarifa kutoka baraza la utawala la Sudan imesema. Pia alipokelewa na maafisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Ethiopia na upelelezi, imeongeza taarifa hiyo.

Daglo ni mkuu wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF), kitengo cha wanamgambo wenye nguvu na wanaoogopewa kilichotuhumiwa kufanya mauaji katika mkoa wa magharibi wa Darfur.

Uhusiano kati ya Khartoum na Addis Ababa umezorota kutokana na vita vya eneo juu mzozo wa mpaka wa mkoa wa Al-Fashaqa, ambako wakulima wa Ethiopia wanalima katika ardhi yenye rutuba ambayo Sudan wanadai ni mali yao.

Kumekuwa na mapigano ya kinyama ya mara kwa mara yakiendelea kati ya pande mbili katika miaka ya karibuni.

Al-Fashaqa pia inapakana na mkoa wa Tigray wenye mgogoro nchini Ethiopia, na maelfu ya wakimbizi wa Ethiopia wamekimbilia Sudan kutokana na vita.

Mwezi Novemba, jeshi la Sudan lilisema wanajeshi sita waliuawa katika shambulizi ililofanywa na makundi yenye silaha na wanamgambo wanaohusishwa na jeshi la Ethiopia, taarifa ilikanushwa na Addis Ababa, wakiwalaumu waasi kutoka Tigray.

Sudan, pamoja na Misri, ziko katika mvutano mkubwa juu ya bwawa kubwa la Ethiopia lilioko katika Mto Blue Nile.

Nchi hizo mbili zilizoko eneo la chini la mto huo, zinazotegemea mto huo kwa ajili ya sehemu kubwa ya matumizi ya maji, wanaliona Bwawa la Ethiopia Renaissance kama ni tishio kwa maisha yao.

Wote Khartoum na Addis Ababa wamegubikwa katika migogoro.