Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 21:53

Serikali ya Ethiopia yamshutumu Ghebreyesus baada ya kuikosoa


Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Serikali ya Ethiopia imeandika barua kwa Shirika la Afya Duniani, ikimshtumu mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus kwa kile imekitaja kama kutelekeza majukumu yake vibaya.

Ghebreyesus, ambaye ni raia wa Ethiopia, ameshutumiwa na serikali yake baada ya kuikosoa kwa kudai kwamba imezuia misaada ya kibinadamu kufikia watu katika eneo la Tigray, kutokana na vita eneo hilo.

Serikali ya Ethiopia ilimteua Tedros Adhanon Ghebreyesus kuongoza shirika hilo la Umoja wa Mataifa miaka minne iliyopita, lakini imesema kwamba ameshindwa kutekeleza majukumu yake kulingana na maadili inavyotarajiwa kutoka kwa ofisi yake.

Imemshutumu kwa kuingilia mambo ya ndani ya Ethiopia.

Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imesema kwamba Tedros ameeneza habari potofu na kuharibu sifa, uhuru na uaminifu wa shirika la afya duniani.

WHO haijajibu barua ya Ethiopia.

Ethiopia inataka bodi ya WHO yenye wanachama 34 kumchunguza Ghebreyesus, ikisema kwamba amekosa kutekeleza majukumu yake kwa njia inayostahiki na kwa kuwajibika.

Barua hiyo imetumwa siku chache kabla ya bodi ya WHO kuandaa kikao muhimu cha 150, kuthathmini utendakazi wa Dkt Tedros kwa muhula wa pili ofisini.

Bodi hiyo itakutana kuanzia tarehe 24 hadi 29, mwezi huu wa Januari, kukubaliana kuhusu agenda ya shirika hilo la afya duniani, Pamoja na kuangazia wagombea wa nafasi ya mkurugenzi mkuu wa shirika hilo katika uchaguzi utakaofanyika mwezi May wakati wa kongamano kuu la 75 la WHO.

Ghabreyesus pekee ndiye ameonyesha nia ya kuongoza shirika hilo la afya na shughuli ya kuwateua wagombea ilikamilika mwezi Novemba, baada ya Kenya, Rwanda na Botswana kuiandikia barua bodi ya shirika hilo kuidhinisha uongozi wake.

XS
SM
MD
LG