Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:08

Ripoti ya HRW: Watigray waliofukuzwa Saudi Arabia wakamatwa walipowasili Ethiopia


Prince Mohammed bin Salman
Prince Mohammed bin Salman

Maelfu ya watu kutoka jamii ya Tigray, waliofukuzwa kutoka Saudi Arabia wanaripotiwa kukamatwa, kutendewa vibaya na hata wengine hawajulikani walipo nchini Ethiopia.

Hii ni kulingana na ripoti ya shirika la Human Rights Watch.

Ripoti hiyo inasema kwamba watu wa Tigray walioingia Saudi Arabia kama wahamiaji wasiokuwa na vibali, walinyanyaswa sana wakiwa kizuizini baada ya kurudishwa Ethiopia kutoka Saudi Arabia.

Hatua ya kuwarudisha Ethiopia wahamiaji hao ilifanyika wakati wanajeshi wa serikali ya Ethiopia wanapambana na wapiganaji wa Tigray.

Vita kati ya wanajeshi wa Ethiopia na wapiganaji wa Tigray vilianza Novemba 2020.

Maelfu ya watu wa Tigray walirudishwa nchini mwao mwaka uliopita, kati ya Desemba 2020 na mwezi Juni mwaka uliopita, baada ya kufikiwa kwa makubaliano kati ya Ethiopia na Saudi Arabia.

Ripoti ya human rights watch inasema kwamba watu kutoka jamii ya Tigray walizuiliwa katika sehemu tofauti mjini Addis Ababa na kwingineko, kinyume na matakwa yao.

Baadhi yao walipigwa kwa kutumia mipira na bakora.

XS
SM
MD
LG