Vikosi vya Tigray vinavyo pambana na vikosi vya serekali kuu ya Ethiopia vimejitoa kutoka eneo la jirani la kaskazini mwa Ethiopia.
Msemaji wa Tigray, Jumatatu, amesema na hii ikiwa ni ishara ya kuelekea uwezekano wa kusimamisha mapigano baada ya baada ya jeshi la Ethiopia kutwaa himaya zaidi.
Vita vya miezi 13 katika taifa hilo la Afrika la pili kwa idadi kubwa ya watu vimedhoofisha eneo hilo ambalo tayari lilikuwa na migogoro, na kuzalisha wakimbizi 60,000 waliokimbilia Sudan, kuondolewa wanajeshi wa Ethiopia waliokuwa Somalia, na kurejesha vikosi vyake vilivyokuwa katika taifa jirani la Eritrea.
Gatachew Reda ambaye ni msemaji wa TPLF, amesema kwamba wamemaliza kuviondoa vikosi vyao kutoka katika maeneo ya Amhara na Afar.
Akiandika katika ujumbe wa Twitter, ameongeza kusema kwamba TPLF inatarajia kujiondoa kwake kutaiwezesha jumuiya ya kimataifa kuweka msukumo kwa serekali ya Ethiopia, na taifa jirani la Eritrea, washirika wa katika mgogoro kusimamisha oparesheni za kijeshi zinazofanywa katika eneo la Tigray.