Tangazo hilo limetolewa siku moja baada ya vyanzo vya habari kutoka mashirika yanayotoa misaada ya kibinadamu kusema kwamba mashambulizi ya angani yameharibi kituo muhimu sana cha kusambaza nguvu za umeme.
Msemaji wa serikali Legesse Tulu amewaambia waandishi wa habari kwamba serikali itachukua hatua zote zinazowezekana kuhakikisha kwamba wapiganaji wa Tigray – TPLF sio tisho kwa serikali.
Lagesse amesema kwamba mashambulizi ya jeshi la Serikali yamebabisha maafa na uharibifu mkubwa kwa kundi la TPLF kiasi kwamba hawawezi kuendelea na malengo yao.
Wapiganaji wa Tigray wamekuwa wakipigana na wanajeshi wa serikali kwa mda wa mwaka mzima sasa.
Mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganani wa Tigray yamekuwa yakiendelea kwa mda wa mwaka mzima. Yamepelea maelfu ya watu kukosa makao.