Mwakilishi Mrepublikan Matt Gaetz aliwasilisha hoja Jumatatu jioni kulazimisha ipigwe kura ya kumuondoa McCarthy, akisema amechoshwa na uongozi wa McCarthy baada ya McCarthy kushindwa kupitisha mswaada wa ufadhili wa serikali wiki iliyopita kwa kuzingatia vipaumbele vya matumizi ya Waconservative.
Hakuna spika wa Baraza la Wawakilishi ambaye aliyewahi kuondolewa katika nafasi yake.
“Kama ningehesabu ni mara ngapi watu wametaka kuniondoa katika nafasi yangu, ningekuwa tayari nimeshaondoka siku nyingi,” McCarthy aliwaambia waandishi wa habari Jumanne asubuhi.
Kura ya kumuondoa McCarthy itahitaji wingi mdogo katika Baraza la Wawakilishi lenye wajumbe 435. Warepublikan wanadhibiti baraza hilo kwa idadi ya wajumbe 221 dhidi ya 212 wapinzani wa Wademokratik.
Ikitegemea ni wawakilishi wangapi wanahudhuria kikao na upigaji kura katika ukumbi wa Bunge, McCarthy anaweza kumudu kubaki katika nafasi yake kama ni wabunge Warepublikan sita hawatampigia kura.
Ni ripoti ya mwandishi wa VOA, Katherine Gypson.