Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 21:52

Spika McCarthy anakabiliwa na tishio kwa nafasi yake ya uongozi


Spika wa bunge la Marekani, Kevin McCarthy akizungumza na waandishi wa habari kwenye jengo la bunge baada ya kura ya kuepuka kufungwa shughuli katika serikali kuu.
Spika wa bunge la Marekani, Kevin McCarthy akizungumza na waandishi wa habari kwenye jengo la bunge baada ya kura ya kuepuka kufungwa shughuli katika serikali kuu.

Gaetz aliwasilisha hoja Jumatatu na hivyo kuwepo na utaratibu wa  upigaji kura katika siku zijazo. McCarthy alionekana kutupilia mbali changamoto hiyo katika maelezo yake  kwenye mtandao wa X. Kura ya kumuondoa McCarthy itahitaji wingi mdogo wa kura katika bunge lenye wajumbe  435.

Spika wa bunge la Marekani Kevin McCarthy anakabiliwa na tishio kwa nafasi yake ya uongozi baada ya mwanachama mwenzake wa chama cha Republican, mbunge Matt Gaetz kuwasilisha hoja ya kulazimisha kura ya kumuondoa McCarthy.

Gaetz aliwasilisha hoja hiyo Jumatatu na hivyo kuwepo na utaratibu wa upigaji kura katika siku zijazo. McCarthy alionekana kutupilia mbali changamoto hiyo katika maelezo yake kwenye mtandao wa X, aliandika, “Ilete tu.” Kura ya kumuondoa McCarthy itahitaji wingi mdogo wa kura katika bunge lenye wajumbe 435.

Wa-Republican wanashikilia udhibiti wa bunge hilo kwa wingi wa viti 221 kwa 212 dhidi ya wabunge wa chama cha Democratic. Changamoto kutoka kwa Gaetz ilikuja siku chache baada ya McCarthy kutegemea kura kutoka katika kambi ya wa-Democratic kupitisha hatua ya ufadhili wa muda mfupi na kuepuka kufungwa kwa serikali kuu.

McCarthy alishika nafasi ya spika wa bunge mwezi Januari baada ya mizunguko upigaji kura wa mara kadhaa ambapo ilishuhudiwa Gaetz na Wa- Republican wengine wakipinga azma yake ya kugombea kiti hicho.

Moja ya makubaliano ambayo yalipelekea McCarthy kukubalika ni kufuatia kukubali kuruhusu mwanachama yeyote kuitisha kura ya kumuondoa spika. Hakuna spika wa bunge aliyewahi kuondolewa kwenye wadhifa huo.

Forum

XS
SM
MD
LG