Matumaini ya Afrika yatoweka katika Kombe la Dunia

  • Abdushakur Aboud

Wachezaji wa Uruguay washeherekea ushindi wao dhidi ya Ghana.

Wawakilishi wa mwisho wa Afrika katika mashindano ya kombe la dunia Ghana wametolewa kufuatia mikwaju ya penalti ambapo Uruguay wamefunga penalti nne na Ghana wamepata penalti mbili.

Mchezo huo wa robo fainali ulilazimika kwenda katika muda wa nyongeza baada ya timu hizo kumaliza dakika mia moja na ishirini zikiwa sare ya bao moja kwa moja.Asamoah Gyan ndiye atakumbukwa zaidi na Ghana baada ya kukosa penalti katika dakika ya mwisho ya nyongeza kufuatia mmshambuliaji wa Uruuguay Soures kuudaka mopira uliokuwa unakwenda wavuni.

Nahodha wa Ghana John Mensah na Domonic Adiyah ndio waliokosa penalti kwa uapnde wa Ghana.
Uruguay sasa watachuana na Uholanzi katika hatua ya nusu fainali.

Katika hatua nyingine goli moja la kujifunga na jingine la kona yameiondoa Brazil katika mashindano ya kombe la dunia mwka huu mbele ya Uholanzi katika mchezo wa robo fainali ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini.
Kiungo wa Brazil Filipe Melo licha ya kujifunga lakini pia alionyeshwa kadi nyekundu na kigharimu timu yake ambayo awali ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo.

Kiungo wa Inter Milan ya Italia Wesley Sneider ndiye aliyefunga bao lililoiondoa Brazil katika mashindano hayo na kocha wake Carlos Dunga huenda huo ndio ulikuwa mchezo wake wa mwisho kuiongoza Brazil.