Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 17:59

Afrika Kusini tayari kwa Kombe la Dunia


Mashabiki wa kansdanda wa Afrika Kusini.
Mashabiki wa kansdanda wa Afrika Kusini.

Mashabiki wa kandanda wa Afrika Kusini ni miongoni mwa mashabiki wenye kushangiria kwa nderemo na fujo kuliko wengine wengi duniani. Kwao wao ni sherehe na ikiwa wanashinda au kushindwa huwa wanasherekea kwa nyimbo, dansi na makelele.

Wauzaji bendera wanafanya biashara nzuri kabisa kwani kila mtu anafuata wimbi la wengi. Bendera kutoka mataifa 32 yanayoshindana katika kombe zinaonekana zikipepea kwenye magari, majumba na ofisini, lakini iliyomashuhuri zaidi ni ya Afrika Kusini bila shaka.

Kinyago cha mwaka huu 2010 amepewa jina la Zakumi, anafanana na chui aliyevazwa joizi ya kandanda akiwa na nywele zilizosukwa za rangi ya kijani. Amekua mashuhuri anapozuri nchi nzima kuhamasisha mchezo huo.
Saddam Maake anajitaja kua shabiki wa kwanza wa timu ya Afrika Kusini. Amehudhuria takriba michuano yote akiwa ameva na kujipaka rangi za timu ya taifa, kijani na manjano kutoka kichwa hadi vidole vya miguu. Maake anasema “ninapenda sana kandanda mimi ni mtumwa wa kandanda nina kunywa kandanda, nina lala kandanda nina kula kandanda ndiyo maana ninapenda kandanda”.

Miongoni mwa mavazi ya mashabiki wakuu ni kofia inayojulikana kwa jina la Makarapa inatengenezwa na plastiki na kufanana na zile kofia wachimba migodi huvaa, halafu huchorwa mipira, bendera au picha za wachezaji mashuhuri.
Alfred Baloyi ni msani na shabiki mwengine mkubwa aliyetengeneza makarapa ya kwanza miaka 30 iliyopita baada ya kushuhudia shabiki mmoja akipigwa kichwa na chupa iliyotupwa wakati wa mchuano wa kandanda.

Baloyi anasema, “ninapokwenda uwanjani ninaiva ili kukinga kichwa change. Na hivyo kinanza kuchora mambo tofauti na kila ninapokwenda uwanjani watu walikua wanaipenda na hivyo ndivyo imekuja kua mashuhuri”.
Kofia hiyo ilianza kua mashuhuri na hapo akanaza kuziuza. Hivi sasa wasani kadhaa wameiga kazi yake na wanatengeneza maelfu ya kofia kila mwezi na kuwauzia wateja kote duniani.

Chombo kingine cha kusababisha nderemo uwanjani ni aina ya pembe ndefu iliyozusha utata mkubwa, inayojulikana kama Vuvuzela, ambayo hutoa sauti moja tu, lakini wakati maelfu ya watu wanapoipuliza kwa wakati mmoja hutoka sauti kubwa ya makelele na hata inaweza kukera sana timu za upinzani. Baadhi ya wachezaji wa kigeni na vituo vya televisheni vilitaka pembe hiyo ipigwe marufuku lakini FIFA, shirikisho la kandanda Duniani ilikata ikisema hiyo ni sehemu ya shamra shamra za kandanda barani afrika.

Na hata kuna dansi maalum iliyotungwa kwa ajili ya Kombe la Dunia inajulikana kama Diski. Ni dansi inayoiga jinsi wachezaji kandanda wanavyocheza na kuchenga uwanjani.

Ingawa wageni wengi wanahisi shangwe na nderemo hizo ni kero kwa kiwango fulani kusikia, hata hivyo mashabiki wengi wa kigeni wanasema wanapenda hali hiyo kwa sababu ni kusherehekeea kandanda. Na barani Afrika kusherekea kandanda ni kufanya makelele.

XS
SM
MD
LG