Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 17:48

Brazil yaanza kwa ushindi dhidi ya Korea Kaskazini


Luis Fabiano wa Brazil akiruka juu ya golikipa wa Korea Kaskazinii Myong Guk, baada ya mwenzake Maicon kupachika bao la kwanza. (Picha AP /Andre Penner)
Luis Fabiano wa Brazil akiruka juu ya golikipa wa Korea Kaskazinii Myong Guk, baada ya mwenzake Maicon kupachika bao la kwanza. (Picha AP /Andre Penner)

Brazil yaanza vizuri kwa kuishinda Korea Kaskazini 2-1.

Brazil moja ya timu yenye matumaini makubwa ya kutwaa Kombe la Dunia imeanza vizuri michuano hiyo kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Korea Kaskazini. Zikiwa katika kundi linalojulikana kama kundi la kifo – yaani kundi G lenye nchi za Brazil, Ureno, Ivory Coast na Korea Kaskazini – Brazil na Korea Kaskazini zilichuana vikali, huku wakorea wakitoa ushindani mkali dhidi ya Brazil. Hadi kipindi cha kwanza hakuna aliyepata bao.

Lakini mambo yalibadilika katika kipindi cha pili pale Maicon alipoipatia Brazil bao la kwanza kwa mkwaju mkali kutoka pembeni kabisa kwenye dakika ya 55. Elano aliipatia Brazil bao la pili katika dakika ya 72 na J. Yun Nam aliipatia Korea Kaskazini bao la kufutia machozi katika dakika ya 89. Brazil sasa inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi tatu, ikifuatiwa na Ivory Coast and Ureno zenye pointi moja moja baada ya kutoka sare 0-0 mapema.

Mechi ya Ivory Coast na Ureno ilikuwa ya kusisimua sana na baadhi ya wachambuzi wanasema huenda Ivory Coast ndio timu iliyoonyesha mchezo mzuri kuliko timu nyingine zote za Afrika mpaka sasa. Mshambuliaji hatari wa Ivory Coast Didier Drogba aliingia katika kipindi cha pili cha mechi hiyo na kuleta msisimko mkubwa katika lango la Ureno – alipotoa krossi mbili ambazo zingeweza kuipatia Ivory Coast goli katika dakika za mwisho mwisho.

Walinzi wa Ivory Coast pia walicheza vizuri na kumbana vikali mshambuliaji nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo ambaye hakuweza kupata nafasi inayoweza kusema ni ya wazi kabisa kupata goli isipokuwa katika dakika za awali kabisa alipoachia mkwaju mkali kutoka nje ya penalty box lakini golikipa wa Cameroon akapanchi mpira huo nje.

Mapema Jumanne asubuhi New Zealand ilipata goli la kusawazisha katika dakika tatu za nyongeza na kupata sare ya 1-1 na Slovakia katika mechi ya kundi F huko Rustenburg. Winston Read wa New Zealand alifunga bao hilo kwa kichwa.

Hadi hapo Slovakia ilikuwa inaongoza kwa bao lilifungwa na Robert Vittek kwa kichwa katika dakika ya 50. Vittek alikosakosa kufunga goli jingine katika dakika ya 69 lakini mlinzi wa New Zealand Mark Paston alikuwa macho. Kwa matokeo hayo ni kwamba timu zote za kundi F zina pointi moja moja hadi sasa baada ya timu nyingine mbili za kundi hilo Italia na Paraguay kutoka sare 1-1 Jumatatu.

XS
SM
MD
LG