Gavana Nigeria aunda kikosi cha kupambana na magenge ya uhalifu

Msichana aliyekuwa ametekwa akijiandaa kuungana na familia yake katika jimbo la Zamfara Machi 3, 2021. Picha na Aminu ABUBAKAR / AFP.

Gavana wa jimbo lililokumbwa na machafuko amezindua kikosi chenye askari 2,600 kupambana na magenge ya wahalifu wanaofanya ugaidi Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo .

Jumbo hilo Masikini maskini la Zamfara ni moja ya maeneo kadhaa yanayokumbwa na wahalifu wanaojulikana kama majambazi wanaovamia na kupora vijiji, kuua na kuchomanyumba.

Magenge hayo yana kambi katika msitu mkubwa ulioko kati ya majimbo ya Zamfara, Katsina, kaduma na Niger, na yamekuwa yakiteka nyara makundi ya wanafunzi katika miaka ya hivi karibuni.

Awali katika jimbo la Zamfara lilipiga marufuku makundi ya kujitolea yaliyokuwa yakipambana kwa kuhofia yalikuwa wakiongeza ghasia na wataalamu walitoa kauli za uoga, lakini mamlaka zimesema kundi hili jipya limepewa mafunzo kuzuia unyanyasaji.

Gavana Dauda Lawal Dare ametangaza kuundwa kwa Jumuiya ya ulinzi katika jimbo la Zamfara katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya serikali huko Gusau siku ya Jumatano.

“Leo. Kundi la kwanza la walinzi wa kujitolea 2,645 wanahitimu” picha za video iliyorushwa na chombo cha utangazaji cha Nigeria ikimuonyesha Dare aliuambia umati wa watu waliokuwa wakishangilia.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP